Timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara kesho
itashuka dimbani huko nchini Ethiopia kukipiga dhidi ya Somalia katika mchezo
wa Kundi A wa michuano ya Chalenji inayohusisha timu kutoka nchi za Afrika
Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA Challenge Cup.
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa nane mchana.
Tayari kikosi cha Taifa Stars kipo nchini Ethiopia
kikisubiri mashindano hayo chini ya kocha mkuu Abdallah ‘King’ Kibadeni ‘Mputa’
Asilimia kubwa ya wachezaji wanaounda kikosi hicho
wanatoka Taifa Stars, kikosi ambacho kilicheza na Algeria, lengo likiwa
kumpunguzia kocha kazi kwa sababu wachezaji wengi wameiva kimazoezi.
![]() |
| Kibadeni |
Nayo Kenya watakipiga na mabingwa wa kihistoria, Uganda
kesho hiyo hiyo majira ya jioni.
Mechi za mzunguko wa kwanza wa makundi
zitakamilishwa keshokutwa ambapo Sudan Kusini watamenyana na Djbouti kabla ya
Sudan na Malawi kufuatia baadaye.
Baada ya mechi za makundi kufikia tamati, Robo
Fainali zitafuatia Novemba 30 zikihusisha timu mbili za juu kutoka kila kundi
na washindi watatu bora wawili kwa makundi yote.
Nusu Fainali zitafanyika Desemba 2 na 3, wakati
mechi za kusaka Mshindi wa tatu na Fainali zitafanyika Desemba 5, mwaka huu na
huo utakuwa mwisho wa mashindano.
RATIBA
Novemba
21, 2015
Burundi Vs Zanzibar Saa 8:00 mchana
Ethiopia Vs Rwanda Saa 11:00 jioni
Novemba
22, 2015
Somalia Vs Tanzania Saa 8:00 mchana
Kenya Vs Uganda Saa 11:00 jioni
Novemba
23, 2015
Sudan v Djbouti Saa 8:00 mchana
Sudan v Malawi Saa 11:00 jioni
MAKUNDI:
Kundi A; Ethiopia, Rwanda, Tanzania Bara na Somalia.
Kundi B; Kenya, Uganda, Burundi na Zanzibar.
Kundi C; Sudan, Sudan Kusini, Malawi na Djibouti.


0 comments:
Post a Comment