NDOA ZA WAANDISHI WA MICHEZO ZAONGOZANA 2015

Ahmed Ally akiwa 'kapozi' na mkewe


Na Arone Mpanduka

Hayawi hayawi na sasa yamekuwa. Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa mwandishi wa habari za michezo Ahmed Ally ambaye ameachana na ukapera na kufunga ndoa jana(Ijumaa).

Ahmed Ally ambaye ni mwandishi wa habari za michezo kutoka katika kituo cha Televisheni cha Star TV na Radio Free Afrika, pia ni mwanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA)

Kitendo cha Ahmed kufunga ndoa hiyo ya Kiislamu kimeongeza idadi ya waandishi wa bahari za michezo waliojitosa na kufunga ndoa kwa mwaka huu.

Miongoni mwa waandishi hao ni Michael Matemanga, Khatim Naheka, Michael Momburi (wote kutoka Kampuni ya Mwananchi Communications Limited) pamoja na Arone Mpanduka (Radio Tumaini) ambaye pia ni mmiliki wa MPANDUKA BLOG.

Disemba 26 mwaka huu, mwandishi mwingine wa habari za michezo Wilbert Molandi anatarajia kufunga ndoa.

Molandi kwa sasa anafanya kazi katika gazeti la michezo la Champion.

Habari za uhakika ambazo MPANDUKA BLOG imezipata zinaeleza kwamba kabla ya mwaka huu kumalizika waandishi wengine wa habari za michezo wataoa na kuolewa.
Mke wa Ahmed Ally katika 'pozi' tofauti tofauti

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment