KILI STARS YAIPELEKA ETHIOPIA ROBO FAINALI CHALENJI

Ethiopia


Bao la kujifunga la beki wa Kilimanjaro Stars Salum Mbonde leo limewasaidia Ethiopia kutinga hatua ya robo fainali baada ya kupata sare ya 1-1 katika mchezo wa mwisho wa kukamilisha hatua ya makundi wa michuano ya Chalenji inayoendelea huko nchini Ethiopia.

Kilimanjaro Stars leo iliingia uwanjani huku ikiwa haina cha kupoteza baada ya kuwa tayari na pointi 6 kibindoni na kufuzu kutinga hatua ya robo fainali isipokuwa ilitaka kushinda ili kulinda heshima.

Kili Stars ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Simon Msuva ambapo bao hilo la pili kwake katika mashindano ya mwaka huu kwa kichwa dakika ya 51 akimalizia krosi maridadi ya beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.


Baada ya bao hilo mnamo dakika ya 90 ndipo Mbonde alipojifunga katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na Mohamed Naser.



Kwa mujibu wa hesabu za kundi hilo la A, Ethiopia ilihitaji sare tu dhidi ya Kili Stars ili isonge mbele na si kinyume na hapo, jambo ambalo limetokea.

Baada ya mechi hiyo, hatua ya robo fainali itaanza rasmi keshokutwa ambapo..

Tanzania Bara Vs Ethiopia

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment