Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametupiwa lawama na
wadau wa klabu ya Arsenal akiwemo gwiji Thierry Henry kutokana na kumchezesha
mchezaji Alexis Sanchez katika mchezo wa jana dhidi ya Norwich na kumsababishia
aumie na kutolewa nje kabla mechi haijaisha.
Alexis Sanchez alipata majeraha madogo katika mchezo
wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Dinamo Zagreb katikati ya wiki, lakini Arsene
Wenger alitamka kuwa Sanchez angekua fiti kucheza mechi ya jana, lakini baada
ya kucheza aliumia na kutolewa nje na sasa anaongeza idadi kubwa ya majeruhi
iliyopo katika kikosi cha Arsene Wenger.
Mkongwe Thierry Henry alimlaumu kocha huyo kwa
kutochukua tahadhari kwa kumuacha nje mchezaji huyo huku akienda mbali zaidi na
kusema kuwa Sanchez alitakiwa kutomaliza mchezo dhidi ya Dinamo Zagreb ulioisha
kwa Arsenal kushinda goli 3-0 ili aweze kumpumzisha.
Kuumia huko kwa Alexis Sanchez ni habari mbaya kwa
mashabiki wa klabu ya Arsenal ambao wanashuhudia timu yao ikiwa na wimbi kubwa
la majeruhi ambapo kiungo Coqueline aliumia wiki iliyopita na kujumuika na
majeruhi wa muda mrefu Jack Wilshere, Danny Welbeck na Thomas Rosicky huku pia
Mikel Arteta na Theo Walcott wakiwa majeruhi

0 comments:
Post a Comment