LICHA YA SARE, TFF KUIPA STARS 'MAMILIONI' YA USHINDI



























Licha ya timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Algeria jioni ya leo, Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi amesema sekretarieti yake itaipatia timu hiyo kiwango cha pesa za ushindi badala ya cha sare.

Akizungumza baada ya mechi kumalizika, Malinzi alisema kwa mujibu wa kanuni Taifa Stars hulipwa kiasi kikubwa cha fedha za motisha pindi inapopata ushindi na kupewa kiasi kidogo zaidi cha pesa pindi inapopata sare.

Amesema kutokana na jitihada kubwa walizoonyesha wachezaji kwenye mchezo wa leo, TFF haitazingatia kanuni hiyo na badala yake itawapatia wachezaji kiasi cha fedha cha ushindi.

“Mbali na bonus ya kikanuni pia wachezaji waliahidiwa kiasi cha shilingi milioni hamsini endapo wangeshinda mchezo huu lakini kiasi hicho nacho tutawapelekea kwenye hoteli ya Serena kama kilivyo”

“Nimetoka kwenye vyumba(vya mapumziko) muda huu, kila mmoja anaangua kilio lakini nimewasihi watulie na kwamba mchezo ujao tutashinda tu,” alisema.
Elius Maguli akishangilia bao lake alilofunga leo


Katika mchezo wa leo, Taifa Stars ilikuwa ya kwanza kupata mabao mawili yaliyofungwa na Elias Maguli (bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 43) na Mbwana Samatta aliyeongeza la pili katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili.

Mnamo dakika ya 71 ya mchezo Islam akarejesha bao la kwanza kwa upande wa Algeria kabla ya mchezaji huyo huyo kusawazisha la pili katika dakika ya 74.

Kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kuondoka kesho kwenda nchini Algeria kwa lengo la kuzoea mazingira mapema kabla ya mchezo wa marudiano wa Jumanne wiki ijayo.
Baadhi ya mashabiki waliokuwepo uwanjani jioni ya leo










Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment