Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi
ameanza kufanya mazoezi katika timu B na anaonekana anakaribia kupona kabisa.
Kocha wa timu B, Gerard Lopez amesema kumekuwa
dalili njema kutoka Messi ambaye amekuwa nje ya uwanja toka alipoumia goti
katika mchezo dhidi ya Las Palmas Septemba 26 mwaka huu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina anategemewa
kuukosa mchezo wa Clasico dhidi ya mahasimu wao Real Madrid Jumamosi hii
kwasababu ya majeruhi lakini Lopez amebainisha Messi amekuwa akifanya mazoezi
na kikosi chake na kuonyesha maendeleo mazuri.
Lopez amesema Messi alikamilisha mazoezi na
alionekana kutokuwa na tatizo lolote hivyo anadhani hizo ni dalili njema. Lopez
aliendelea kudai kuwa anashukuru kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 kufanya
nao mazoezi.

0 comments:
Post a Comment