Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amesema kama
akijiunga na klabu yoyote ya Ligi Kuu Uingereza, basi atahitaji kulipwa kiasi
cha paundi laki 6 kila wiki.
Kwa mujibu wa Gazeti la The Star, Messi amechagua klabu
tatu za Uingereza ambazo angependa kuzichezea ambazo ni Arsenal, Manchester United au Manchester City.
Taarifa zinadai kwamba Messi anaweza kuhama
Barcelona kwasababu ya matatizo mengi anayopata ikiwemo kodi na kesi za
mahakamani.
Lakini pia kiongozi wa ngazi ya juu ya Barcelona
alisema kwamba Messi atacheza Barcelona hadi mwisho wa soka lake.

0 comments:
Post a Comment