SIMBA YAMTEMA MSENEGALI PAPE N'DAW

Pape N'daw


Klabu ya soka ya Simba imeamua kuachana na wachezaji Pape N’daw raia wa Senegal na Simon Sserunkuma kufuatia kuwa na mwenendo mbovu.

Akizungumzia kuachwa kwa wachezaji hao, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha klabu ya Simba Hajji Manara alisema uongozi umeridhia na kuamua kuachana na wachezaji hao baada ya kupokea ripoti ya kocha mkuu Muingereza Dylan Kerr.

Alisema pamoja na kuachana na wachezaji hao, klabu yao ina mipango ya kuwaongeza wachezaji wengine akiwemo Paul Kiongera.

“Pape N’daw na mwenzake si kwamba ni wabaya, wazuri lakini kuna wakati mchezaji anakuwa haendani na programu za kocha na huenda hilo ndilo lililotokea kwao.Tunawashukuru sana wachezaji hawa kwa mchango wao,”alisema Manara.

“Simon amekwishaondoka lakini N’daw bado yupo na tunategemea siku hivi mbili tatu naye atarejea Senegal na jana tu alifanya mazoezi ili kuuweka fiti mwili wake”

MATUKIO YA KUKUMBUKWA YA MSENEGALI PAPE N'DAW KWA NJIA YA PICHA
Hiki ni kiatu ambacho hakiwezi kusahaulika kufuatia mchezaji huyo kukivaa hivi karibuni kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Yanga.Kiatu hicho kilionekana kimechakaa tofauti na hadhi ya mchezaji mwenyewe.


 
Picha kubwa inaonyesha Pape N'daw katikati akizongwa na wachezaji wa Tanzania Prisons waliokuwa wakimshinikiza atoke uwanjani baada ya kukutwa na kitu kiunoni kilichosadikiwa kuwa ni hirizi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliofanyika hivi karibuni jijini Mbeya.Katika mchezo huo Simba ililala kwa kufungwa bao 1-0.Picha ndogo pembeni inaonyesha kitu hicho kilichohisiwa kuwa ni hirizi.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment