Timu ya Taifa Stars usiku huu imeondolewa katika kinyang'anyiro cha kuwania kupangwa kwenye makundi ya kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 baada ya kufungwa mabao 7-0 na wenyeji Algeria.
Katika mchezo huo uliochezwa huko nchini Algeria, kipindi cha kwanza Stars iliruhusu mabao matatu kabla ya kuruhusu mengine manne katika kipindi cha pili huku mawili kati ya hayo yakiwa ni ya penati.
Baada ya kuona ngoma nzito hadi muda wa mapumziko, kocha wa Stars Charles Mkwasa alifanya mabadiliko kwa kumuingiza Aishi Manula na Salum Telela lakini hali bado ilikuwa tete.
Stars imetolewa kwa jumla ya mabao 9-2 kufuatia sare ya mechi ya awali ya 2-2.
- Blogger Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment