TYSON KUPANDA ULINGONI JUMAMOSI HII

Wladimir Klitschko atamuangusha Tyson Fury wakati wawili hao watakapopigana katika mji wa Dusseldorf siku ya jumamosi kulingana na bondia wa uzani mzito nchini Uingereza Anthony Joshua.

Klitschko mwenye umri wa miaka 39 amekuwa bingwa wa dunia katika uzani huo tangu mwaka 2006,akiwa amepigana mapigano 27 na kufanikiwa kuyatetea mataji yake mara 23.

Atakuwa akitetea taji lake la WBA ,IBF na WBO dhidi ya raia wa Uingereza Tyson Fury.

''Itakuwa vyema iwapo Fury atashindfa ,lakini namuunga mkono Klitschko katika raundi ya tano au sita'',Joshua aliiambia BBCsport.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment