Timu ya soka ya Azam FC jioni ya leo imetoka sare ya
bao 1-1 na wenyeji African Sports ya jijini Tanga katika mchezo wa kirafiki
uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Hiyo ni mechi ya pili kwa Azam ambayo inajiandaa na
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hapo juzi Azam ilitoka sare ya 1-1 na Mgambo JKT
katika mechi yake ya kwanza ya ziara hiyo ya kimazoezi jijini Tanga.
0 comments:
Post a Comment