LIGI KUU YA MAREKANI KUHUSISHA TIMU 28

BODI ya magavana wa Ligi Kuu ya Marekani-MLS imeunga mkono mpango wa siku zijazo wa kupanua mashindano hayo kufikia klabu 28, wakati pia wakiunga mkono eneo la uwanja lililopendekezwa na David Beckham jijini Miami.

MLS kwasasa inashikirikisha timu 20, huku mipango iliyopo ikiwa ni kukuza kufikia timu 24 ifikapo mwaka 2020.

Atlanta, Los Angeles na Minnesota ndio timu zinazotarajiwa kuongezeka katika ligi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo huku timu ya Miami FC ambayo itakuwa ikimilikiwa na Beckham ikitajwa kukamilisha orodha ya timu 24 za mpango wa awali.

Kamishna wa MLS Don Garber amesema watafanya utafiti kuona ni jinsi gani wataweza kupanua wigo na kufikisha timu 28 katika siku zijazo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment