![]() |
| Rais wa TPBO Yassin Abdallah |
Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO imesema leo(Dis 9) hakuna kingine watakachofanya zaidi ya usafi.
Akizungumza na MPANDUKA BLOG, Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ustaadh' alisema lazima watekeleze amri ya Rais wa Tanzania John Magufuli kwa sababu haikwepeki.
"Tatizo la Watanzania tumezoea kukaa kizembe zembe tu.Kwa hili ninampongeza Rais Magufuli kwa sababu nchi itakuwa safi"
Alisema TPBO haitakuwa na kazi nyingine zaidi ya kufanya usafi kwenye maeneo yanayowazunguka.
Alitoa wito kwa mabondia na wadau wa masumbwi kufanya usafi.
Usafi siku ya 9 Disemba ambayo Tanzania inaadhimisha kumbukumbu ya Uhuru wa Tanganyika, umekuja kufuatia amri iliyotolewa na Rais Magufuli ili kuzuia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

0 comments:
Post a Comment