AUBAMEYANG AMPIKU YAYA TOURE, TP MAZEMBE KLABU BORA AFRIKA

Pierre Aubameyang amebeba tuzo ya mwanasoka bora Afrika anayecheza soka nje ya bara hilo kwa mwaka 2015 na kumpiga kumbo Yaya Toure.

Toure alibeba tuzo hiyo mara tatu mfululizo na kama angechukua ilikuwa ni mara ya nne mfululizo ambayo ingekuwa ni rekodi.

Aubameyang anakipiga katika kikosi cha Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon ambayo yeye ni nahodha.

Tuzo hizo zimefanyika jijini Lagos nchini Nigeria usiku wa Alhamis na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu katika soka Afrika.

ORODHA KAMILI YA TUZO

MCHEZAJI BORA WA AFRIKA - Pierre-Emerick AUBAMEYANG (Gabon)
MCHEZAJI BORA ANAYECHEZA AFRIKA – Mbwana Aly SAMATTA
MCHEZAJI BORA WA KIKE - Gaelle ENGANAMOUIT (Cameroon)
MCHEZAJI BORA KIJANA - Victor OSIMHEN (Nigeria)
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA VIZURI - Etebo Peter OGHENEKARO (Nigeria)
KOCHA BORA WA MWAKA- Herve RENARD (Ufaransa) – Kocha wa zamani wa Ivory Coast
REFA BORA WA MWAKA - Bakary Papa GASSAMA (Gambia)
TIMU BORA YA TAIFA – Ivory Coast
TIMU BORA YA TAIFA YA WANAWAKE- Cameroon
KLABU BORA YA MWAKA - TP Mazembe (DRC)
GWIJI WA AFRIKA - Charles Kumi GYAMFI (Ghana)
Samuel MBAPPE LEPPE (Cameroon)

KIKOSI BORA AFRIKA
Kipa: Robert Muteba KIDIABA (DRC)
Mabeki: Serge AURIER (Ivory Coast), Aymen ABDENNOUR (Tunisia), Mohamed MEFTAH (Algeria)
Viungo: Andre AYEW (Ghana), Yaya TOURE (Ivory Coast), Sadio MANE (Senegal), Yacine BRAHIMI (Algeria),    
Washambuliaji: Mbwana Aly SAMATTA (Tanzania), Pierre-Emerrick AUBAMEYANG (Gabon), Baghdad BOUNEDJAH (Algeria)

WACHEZAJI WA AKIBA;
Djigui DIARRA (Mali)
Azubuike OKECHUKWU (Nigeria)
Kelechi NWAKALI (Nigeria)
Zinedine FERHAT (Algeria)
Adama TRAORE (Mali)
Victor OSIMHEN (Nigeria)
Kermit ERASMUS (Afrika Kusini)
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment