Na Arone Mpanduka
Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya Simba, Dylan
Kerr amesema bado yupo jijini Dar es salaam akisubiri malipo yake ikiwemo
mshahara wa miezi miwili iliyopita.
Akizungumza kwa njia ya simu na MPANDUKA BLOG, Kerr
alisema hangependa kuzungumzia sana masuala yake na klabu hiyo kupitia vyombo
vya habari.
“Sitaki kuzungumzia sana suala la kufukuzwa kwangu
lakini kwa kifupi bado nipo nasubiri viongozi wangu waniite ili tumalize suala
hili,”alisema.
Alisema bado anafuatilia malipo yake ikiwemo
mishahara ya miezi miwili ambayo uongozi wa Simba ulikuwa haukumlipa.
“Bado nafuatilia malipo yangu, sijalipwa miezi
miwili kwa hiyo naomba uniache.Sipendi kuongea sana,” alisisitiza
Hii ina maana kwamba Muingereza huyo alifanya kazi
ya kujitolea katika miezi ya Novemba na Disemba mwaka jana, jambo ambalo huenda
likawa limesababisha timu kucheza bila ya morali.
Kerr ameiongoza Simba katika mechi 13 za Ligi Kuu
Bara na nane kati ya hizo alishinda, sare tatu na alipoteza mbili.
Kwa upande wa mechi za jumla tangu atue nchini
kuinoa timu hiyo, Kerr ameiongoza Simba jumla ya mechi 30 ambapo 19 kati
ya hizo alishindsa na kufungwa mechi 5 huku 6 ikiwa ni sare.

0 comments:
Post a Comment