FAINALI ZA CHAN KUANZA LEO

Michuano ya nne ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani kwa mwaka 2016 maarufu kama CHAN yataanza kutimua vumbi leo huko nchi Rwanda.

Michuano hii ya Chan inashirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani tu, huku mataifa kumi na sita yakichuana kuwania ubingwa huo wa Afrika.

Viwanja vinne vitatumika katika michuano hii ya Chan, ambavyo ni Uwanja wa Amahoro wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 ulipo katika jiji la Kigali, pia upo uwanja wa Stade Huye uliopo katika mji wa Butare ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.

Uwanja mwingine utakatumika ni ule Regional Nyamirambo unaopatika Kigali wenye uwezo wa kupokea watazamaji 22,000, pia uwanja mwingine utakaotumika katika michuano hii ni ule Umuganda ulioko Gisenyi ukichukua washabiki wa soka wapatao 5,000.

Wenyeji Rwanda wako kundi A wakiwa na mataifa ya Gabon, Morocco, Ivory Coast watatumia viwanja vya Amahoro na Stade Huye.

Kundi B lina timu za DR Congo, Angola, Cameroon na Ethiopia timu hizi pia zitatumia viwanja vya Amahoro na ule wa Stade Huye.

Katika kundi D kuna timu za Tunisia , Nigeria, Niger na Guinea timu hizi zitachuana katika viwanja vya Regional Nyamirambo na ule wa Umuganda.

Mataifa ya Zimbabwe Mali Uganda pamoja na Zambia wao wako kundi D, timu hizi zitatumia viwanja vya Umuganda na Regional.

Michuano hii itafikia tamati Februari 7 kwa mchezo wa fainali itakaopigwa kwenye dimba la Amahoro Jijini Kigali.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment