Kamati ya kuratibu mashindano ya urembo ya Miss Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake Juma Pinto imetangaza kujitoa kwenye jukumu la kuratibu mashindano hayo leo baada ya kupishana katika baadhi ya mambo ya kiutendaji ya kamati hiyo.
Kamati hiyo ikiwa na viongozi wakiwemo Jokate Mwengelo, Juma Pinto na Gladys Shao imetangaza maamuzi hayo leo wakati ikiongea na wanahabari jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Juma Pinto amesema kuna mambo bado hayajatakaswa hasa kuhusiana na skendo ya kughushi umri iliyoitafuna kamati iliyopita, hivyo wanahofu kwamba doa hilo litaendelea kuwachafua.
Mwaka juzi mashindano hayo yalikumbwa na skendo ya kughushi umri kwa aliyekuwa Miss Tanzania kwa wakati huo Sitti Mtemvu, jambo lililomfanya avue taji na kumpa Lilian Kamazima.
Kama hiyo haitoshi Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa BASATA iliyafungia mashindano hayo kwa kipindi cha miaka miwili.
Skendo hiyo iliilazimu kamati iliyopita chini ya Hashim Lundenga kujivua gamba na kuwakabidhi jukumu Juma Pinto na jopo lake.

0 comments:
Post a Comment