KLOPP AVUNJA MIWANI WAKATI AKISHANGILIA BAO

Kocha Jurgen Klopp wa Liverpool jana alijikuta akiharibu miwani yake mara baada ya kujumuika pamoja na wachezaji wake kushangilia goli la ushindi katika dakika za mwisho za mchezo wao dhidi ya Norwich uliomalizika kwa ushindi wa magoli 5-4.

Adam Lalana alifanikiwa kuwa shujaa wa mchezo mara baada ya kufunga kwa shuti kali dakika ya 95 ya mchezo dakika chache kabla ya Sebastian Bassong kuisawazishia Norwich na matokeo kuwa goli 4-4.

Kocha Jurgen Klopp anasema ni mara ya pili sasa anaharibu miwani yake kwani anakumbuka Nuri Sahin wakiwa Borussia Dortmund alimrukia wakishangilia ushindi dhidi ya Bayern Munich, na jana ikawa ni Adam Lalana.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment