SAMATTA AKANUSHA KUFUMWA NA MREMBO HOTELINI

Hatimaye Mbwana Samatta ameamua kukanusha taarifa zinazodai kwamba alifumwa na mmoja kati ya warembo wanaotikisa nchini kwa sasa Asha Salum maarufu kama Kidoa.

Kwa mujibu wa gazeti la udaku la Ijumaa lililotoka leo, Samatta ambaye ni kinara wa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Jumapili iliyopita alibambwa kwenye hoteli ya Girrafe iliyopo Mbezi jijini Dar es salaam akiwa amekaa mkao wa kimahaba na nyota huyo huku wakizungumza masuala yao.

Lakini kupitia ukurasa wake wa Istagram hii leo, Samatta amekanusha habari hizo na kumlaumu mwanadada huyo kwamba amefanya mpango wa kibiashara ili achafue jina lake.

Samatta alikiri kwamba msichana huyo ni rafiki yake wa kawaida kwa kipindi kirefu lakini si mpenzi wake.

Alisema baada ya kurejea kutoka nchini Nigeria, msichana huyo alionekana kumlazimisha kupiga nae picha na hata kumtaka ampakie kwenye gari yake, kitu ambacho alifanya bila kujua nia yake.

KILICHOANDIKWA GAZETINI

ALICHOJIBU SAMATTA

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment