SAMATTA ATETA NA JK, AMZAWADIA JEZI

Mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Mbwana Samatta leo amekutana na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete na kutoa shukrani zake.

Samatta na Kikwete walikutana asubuhi ya leo kwenye makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi yaliyoko mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam.

Samatta amemshukuru Rais huyo mstaafu kwa moyo aliompa wakati walipokutana nchini Congo DR, enzi hizo akiwa Rais wa Tanzania.

Naye mheshimiwa Kikwete amempongeza Samatta kwa juhudi alizofanya na kumfanya apate tuzo hiyo.

Mbali na hayo Samatta alimkabidhi Kikwete jezi namba 9 iliyoandikwa neno SAMATTA mgongoni.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment