Serikali imesema ipo tayari kuingilia kati mchakato wa usajili wa Mbwana Samatta wa kucheza barani Ulaya endapo kutatokea vikwazo kati ya klabu ya TP Mazembe na Genk ya nchini Ubelgiji.
Akizungumza jioni ya leo na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Kempiski jijini Dar es salaam, Waziri wa Wizara ya Habari Utamaduni, Wasanii na Michezo Nape Nnauye alisema amepokea agizo kutoka kwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa kwamba Serikali iko tayari kumsaidia mchezaji huyo katika harakati zake za kucheza nje ya Afrika.
" Hili ni agizo rasmi kutoka kwa Waziri mkuu kwamba Serikalu itakuwa bega kwa bega na mchezaji huyu na itaingilia kati pale itakapoona kuna vikwazo katika mchakato wake wa usajili barani Ulaya," alisema.
Hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu kati ya klabu ya TP Mazembe Genk kuhusiana na dau stahiki ambalo litamtoa Samatta katika klabu hiyo na kwenda Ulaya.

0 comments:
Post a Comment