VENUS WILLIAMS ABURUZWA AUSTRALIAN OPEN



Mchezaji nyota wa mchezo wa tenisi kutoka nchini Uingereza Johanna Konta amemshinda nyota machachari wa mchezo huo Venus Williams kwa seti 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili ya shindano la tenisi la Australian Open mjini Melbourne.

Konta, 24, alipata ushindi kwa kutumia dakika 79 huku bingwa wa Grand Slam Williams.

Baaada ya mchezo huo kumalizika na Konta kushina alisema baada ya kuona Droo ilipofanywa na akaona alikuwa amepangwa kucheza na Venus aliomba afanye vizuri bila kufungwa mapema.

Konta, aliyefika hatua ya 16 bora katika US Open mwaka 2015, sasa atakutana na mshindi kati ya Carina Witthoeft na Saisai Zheng, katika raundi ya pili.

Konta aliyeorodheshwa nambari 47 duniani, alikuwa akicheza mara ya kwanza katika Australian Open na ndiye mwanamke Mwingereza pekee aliyesalia katika droo ya mashindano ya mchezaji mmoja mmoja baada ya Heather Watson kushindwa Jumatatu.

Kwa upande wa wanaume mchezaji Andy Murray pia alishinda katika mchezo wake.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment