Baada ya kufungwa na Swansea mabao 2-1 usiku wa jana,kocha mkuu wa Arsenal, Arsene Wenger ameanza kupuuzia ndoto za ubingwa.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu Uingereza imeifanya Arsenal kubaki nafasi ya tatu baada ya kupoteza mechi ya pili mfululizo.
Wenger alisema “Sipo kwenye nafasi nzuri ya kuongelea mataji usiku huu. Kwa sasa hatutakiwi kuota tena inabidi tuwe wa kweli tu.Nina wasiwasi sana kuhusu matokeo yetu, tumepoteza michezo mitatu na huu ni wakati mgumu sana kwa timu.Haya ni matokeo yanayovunja moyo sana na hali ya wachezaji ipo chini sana”
Arsenal wana mechi ngumu dhidi ya Spurs Jumamosi hii na Wenger aliendelea kusema,“Tuna mechi kubwa tatu zinakuja mbele yetu na tunatakiwa kuendelea kufanya kazi ya msingi na kuonyesha ubora pia.Inabidi turudi nyuma na kufanya kama tulivyokua zamani.Ni bahati mbaya sana usiku wa leo tumetengeneza nafasi lakini tumeshindwa kumalizia”

0 comments:
Post a Comment