YANGA, AZAM KUWAFUATA WAARABU WIKIENDI HII

Na Arone Mpanduka

Timu za soka za Yanga na Azam zinatarajia kuondoka wikiendi hii kwa ajili ya michezo yao ya kimataifa ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika pamoja na Shirikisho.

Azam wanatarajia kuondoka Jumamosi kwenda nchini Tunisia kurudiana na Esperance katika mchezo wa kombe la Shirikisho.

Mchezo wa kwanza Azam ilishinda mabao 2-1 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Azam,Saad Kawemba, Azam itacheza mechi ya marudiano Jumanne ya wiki ijayo.

Nayo Yanga ambayo wiki iliyopita ilibanwa mbavu nyumbani kwa sare ya bao 1-1 na waarabu Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Klabu Bingwa, wataondoka Jumapili kwenda Misri kurudiana nao.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro alisema maandalizi ya safari yao yamekamilika.

"Maandalizi ni mazuri na tutaondoka Jumapili, siku moja tu baada ya kucheza na Mtibwa katika mechi ya Ligi Kuu"
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment