Mwingereza Andy Murray ameanza vyema kutetea taji
lake katika michuano ya Madrid Open kwa ushindi wa seti 7-6 7-3 3-6 na 6-1
dhidi ya Radek Stepanek.
Ilichukua muda wa saa mbili na dakika 16 kwa Murry
kumshinda Stepanek raia wa Czech mwenye miaka 37.
Mapema kwenye mchezo wa awali Muhispaniola Rafael
Nadal alimshinda Andrey Kuznetsov wa Urusi kwa seti 6-3,6-3.
Nadal ambaye alifungwa alipocheza na Murray katika
fainali za mwaka jana anaweza kukutana tena na mpinzani wake huyo katika nusu
fainali za mwaka huu.
Kinara nambari moja wa mchezo huo duniani Novak
Djokovic atashuka dimbani siku ya jumatano kukipiga dhidi ya Borna Coric kutoka
Crotia.

0 comments:
Post a Comment