Siku moja baada ya kutoka sare ya 2-2 na JKT Ruvu,
Azam FC imekumbana na balaa lingine hii leo baada ya kupokwa pointi tatu na
mabao matatu kwa kosa la kumtumia beki wao, Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu
za njano.
Taarifa za uhakika zilizoifikia MPANDUKA BLOG
zinasema katika mechi namba 156 iliyozikutanisha Mbeya City dhidi ya Azam
kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Azam ilimchezesha Nyoni kinyume na sheria huku
wakitambua kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Adhabu hiyo inafuatia ushindi wa Azam wa mabao 3-0
iliyoupata Februsri 20 mwaka huu kwenye dimba la Sokoine Mbeya huku ndani yake
akichezeshwa Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.
Licha ya kushinda Azam wamepoteza mchezo ule na sasa
Mbeya City imepewa pointi tatu na mabao matatu huku benchi la ufundi la Azam likionywa
kuwa makini ili jambo hilo lisiwatokee tena.
Hali hiyo inazidi kuiachia Yanga nafasi ya kutwaa
taji la Ligi Kuu msimu huu.
Taarifa
zaidi zitafuata…
NB;
Pia tegea sikio kipindi cha michezo cha kutoka viwanjani cha Redio Tumaini
kuanzia saa 1;00 hadi 1;30 usiku wa leo kupitia 96.5 FM ama nje ya Dar
www.tumainimedia.com
0 comments:
Post a Comment