ENGLAND YATOLEWA EURO, KOCHA AJIUZULU

Saa chache tu baada ya timu ya kandanda ya Uingereza kutupwa nje ya mashindano ya mwaka huu ya Euro 2016, Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amejiuzulu wadhfa wake.

Hodgson alikuwa ameshuhudiwa Uingereza ikiambulia kichapo cha mabao 2-1 usiku wa jana dhidi ya Iceland katika mkumbo wa 16 bora huko ufransa.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 amekiongoza kikosi hicho cha Uingereza kwa miaka 4 sasa.

Hodgson alichukuwa wadhfa huo kutoka kwa kocha muitaliano Fabio Capello aliyetimuliwa kufuatia matokeo duni.

Hata hivyo kocha huyo hajakuwa na wakati mzuri kileleni mwa Uingereza, Hodgson ameiongoza Uingereza kushinda mechi tatu tu kati ya 11 alizoshiriki katika michuano mikubwa ya dunia .

Lakini kitumbua chake kiliingia mchanga baada ya Iceland - yenye jumla ya watu 330,000 - na moja kati ya timu za mataifa yaliyoorodheshwa ya chini kabisa katika orodha ya FIFA ilipoinyuka Uingereza.

Tangu atwae uongozi wa timu hiyo Hodgson, Uingereza imeshinda mechi 33 kati ya 56 .
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment