'WACHOVU' URENO WAINYUKA CROATIA KATIKA UBORA WAKE

Bao la Ricardo Quaresma kwenye muda wa nyongeza limeipa ushindi Ureno na kuipeleka hatua ya robo fainali ya michuano ya Euro 2016 na itakutana na Poland kwenye mchezo wa robo fainali.

Quaresma aliyetokea benchi alifunga kwa kichwa hatua mbili kutoka golini baada ya golikipa Danijel Subasic kuupangua mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo.

Pambano hilo lilibidi kwenda hadi dakika 120 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Croatia ilikaribia kufunga magoli kupitia Domagoj Vida na Marcelo Brozovic kwa mipira ya vichwa wakati Ivan Perisic yeye shuti lake liligonga wamba.

Mchezo wa robo fainali wa Ureno utachezwa Alhamisi kwenye uwanja wa Stade Velodrome, Marseille.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment