Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel anatarajiwa
kuhudhuria mchezo wa kirafiki dhidi ya Uholanzi usiku wa leo ambao utafanyika kama
ulivyopangwa licha ya timu hiyo kuwa bado katika mshangao wa mashambulizi ya
mauaji jijini Paris.
Msemaji wa serikali amesema Merkel anatarajia kuwepo
uwanjani kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika huko Hanover sambamba na waziri
wa mambo ya ndani Thomas de Maiziere.
Mabingwa hao wa dunia walikuwa wakicheza na Ufaransa
huko Paris Ijumaa iliyopita wakati mashabulizi yalipotokea katika viunga kadhaa
vya mji huo na kusababisha vifo vya watu 129.
Rais wa muda wa Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB,
Reinhard Rauball amesema kikosi cha timu hiyo kinataka kupeleka ujumbe kuwa
hawatatishwa wala kukubali kuendeshwa na magaidi.

0 comments:
Post a Comment