Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), kwa kushirikiana
na mzabuni wa tenda ya elektroniki benki ya CRDB, leo limetangaza tenda ya
kumsaka mshauri wa mfumo wa Elektroniki (Consultant) kwa ajili ya kupitia mapungufu yaliyopo katika mfumo wa
uuzaji tiketi wa elektroniki katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania.
TFF imetangaza tenda hiyo ili kumpata mshauri wa
mfumo huo wa tiketi za elektroniki, ambao ulisamishwa na serikali mapema mwaka
huu mwezi Aprili.
Maombi ya tenda yawasilishwe katika ofisi ya Katibu
Mkuu wa TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam, kuanzia saa 3 asubuhi mpaka
saa 10 jioni siku za kazi Jumatatu mpaka Ijumaa.
Gharama ya fomu ya kuombea tenda ni shilingi laki
moja (100,000), na mwisho wa maombi ni Disemba 17, 2015.
0 comments:
Post a Comment