Timu ya soka ya Chelsea alasiri ya leo ( Nov 29) imeibana mbavu timu ya Tottenham kwa kutoka nayo suluhu ya 0-0 kwenye dimba la White Hart Lane.
Matokeo hayo yameifanya Chelsea kupanda kidogo hadi nafasi ya 14 kwenye msimamo wa Ligi hiyo ya England huku Spurs ikiwa kwenye nafasi ya tano.
Katika mchezo huo mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa alionekana kukerwa na kitendo cha kutoingizwa dimbani licha ya kuambiwa apashe moto misuli yake.
Hasira za Costa zilimfanya wakati fulani avue kizibao chake cha kufanyia mazoezi na kumrushia kocha wake Jose Mourinho.
Baada ya mchezo kumalizika Mourinho alikiri timu yake kuonyesha kiwango kizuri kuwahi kutokea katika msimu huu huku akionekana kukipuuza kitendo cha Costa.
Naye kocha wa Spurs, Pochettino alikisifia kiwango cha Chelsea na kusema kwamba timu yake ni mashujaa kwani imecheza na timu iliyoonyesha ubora ambao haukuwahi kutokea tangu msimu uanze.
- Blogger Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment