![]() | ||||
| Kobe Bryant |
Jahazi la Kobe Bryant na timu yake ya Lakers
limeonekana kuzidi kuzama baada ya usiku wa jana kufungwa na New York Knicks
kwa pointi 99-95 kwenye mchezo wa Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani NBA.
Uwanja mzima ulionekana kumshangilia kwa nguvu pale
Madison Square Garden ingawa Lakers walifungwa.
Ikumbukwe kuwa huo ndio uwanja ambao Kobe alifunga
pointi zake za mwanzo za NBA takribani miaka 20 iliyopita.
Katika kipindi hicho Bryant alifunga pointi 18.
“Naweza kukumbuka mchezo wangu wa kwanza hapa , bila
kujua nini cha kutarajia na ni kipi au ni nini cha kufanya, lakini tu kuwa
katika moja ya viwanja vikubwa na vinavyoheshimika ,”alisema Bryant
James alicheza na mguu mbovu kiais lakini kila
alichofanya hakikutofautiana sana na yule Lebron anayecheza akiwa mzima na
mwenye afya kamili.
Katika mchezo mwingine nyota LeBron James alifunga
pointi 29 na kuonyesha kiwango cha juu
na kuiongoza Cleveland Cavaliers kuichapa Pacers Indiana pointi 101-97
na kufikisha ushindi wao wa sita mfululizo.
“Nilianza
mchezo vema bila maumivu yoyote na vizuri lakini nikagongwa tena katika robo ya tatu hivyo ilikuwa inauma
kwelikweli,” James alisema.
Mchezo mwingine ulishuhudia mchezaji Kevin Durant
akizoa pointi 32 na ribaundi 11 wakati timu yake ya Oklahoma City ikiwapiga
Phoenix Suns 124-103 na kukwepa rekodi ya kupoteza michezo mitau mfululizo.
Russell Westbrook alikuwa na pointi 21, pasi 13 na
ribaundi sita , na Enes Kanter alikuwa na pointi 21.
Eric Bledsoe alikuwa na pointi 28 na pasi 11 kwa upande
wa Phoenix Suns.
Markieff Morris alifunga pointi 19 na T.J. Warren
aliongeza 17 kwa Phoenix, ambayo ilipoteza kwa mara ya tatu katika mechi nne.


0 comments:
Post a Comment