Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Nigeria,
Golden Eaglets imetwaa ubingwa wa Dunia wa vijana wa umri wa huo baada ya
ushindi wa 2-0 dhidi ya Mali jana nchini Chile.
Ushindi huo unamaanisha kwamba Nigeria imetetea taji
lao ililolitwaa miaka miwili iliyopita Falme za Kiarabu (UAE).
Mabao ya haraka haraka ya kipindi cha pili ya Victor
Osimhen na Funsho Bamgboye yalitosha kukihakikishia taji hilo kikosi cha
Emmanuel Amuneke, hilo likiwa taji la tano la dunia kwa U17.
Hii ni mara ya kwanza Nigeria wanatwaa taji hilo nje
ya Asia, baada ya mataji yao ya awali kubeba China mwaka 1985, Japan mwaka
1993, Jamhuri ya Korea mwaka 2007 na UAE mwaka 2013.

0 comments:
Post a Comment