![]() |
| Kikosi cha Taifa Stars kikiwa mazoezini |
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
limetangaza viingilio vya mchezo wa Jumamosi kati ya Tanzania dhidi ya Algeria
utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam bei ya chini kuwa ni
shilingi elfu tano (5,000) tu.
Tiketi za mchezo huo zitaanzwa kuuzwa siku ya ijumaa
katika vituo mbalimbali vinavyotumiwa na TFF kuuzia tiketi, ambapo kiingilio
kingine kitakua ni elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C, huku
kiingilio cha elfu tano kikiwa ni kwa viti vya rangi ya Bluu, Kijani na rangi ya
Machungwa.
Wakati huo huo kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania
‘Taifa Stars’ kinachodhamininiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
kinatarajiwa kurejea nyumbani kesho Jumatano mchana kwa shirika la ndege la
Fastjet tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Algeria siku ya
Jumamosi.
Stars iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini imekua
ikifanya mazoezi kila siku katika uwanja wa Edenvale, ambapo mpaka sasa
wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi na kila mmoja yupo tayari
kwa mchezo wa Jumamosi.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema
vijana wake wapo vizuri kifaya, kifikra na morali ni ya hali juu “wachezaji
wamekua wakifanya mazoezi kwa nguvu na kuonyesha umakini mkubwa” alisema
Mkwasa.
Aidha Mkwasa amewaomba watanzania na wadau wote wa
mpira wa miguu nchini kujitokeza kwa wingi kuwapa sapoti ya kuwashangilia
vijana katika mchezo dhidi ya Algeria Jumamosi, kwani kutawafanya wachezaji
kujisikia wapo nyumbani na kucheza kwa nguvu zaidi.
Wachezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na
Thomas Ulimwengu walioshinda kombe la Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa wiki na
klabu yao ya TP Mazembe wanatarajiwa kuungana na wenzao kambini kesho jijini
Dar es salaam.
Wakati huohuo,
Msafara wa timu ya Taifa ya Algeria (The Desert
Warriors) unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Alhamis kwa ndege binafsi ya
kukodi, ukiwa na jumla ya watu 65 wakiwamo wachezaji 24 tayari kwa mchezo wa
Jumamosi Novemba 14 dhidi ya wenyeji Tanzania katika uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam.
![]() |
| Kikosi cha Algeria |
Kocha mkuu wa timu hiyo Iitakayofikia hoteli ya
Kilimanjaro Hyatt Kempsinki, Christian Gourcuff raia wa Ufaransa ametaja kikosi
cha wachezaji 24, wakiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya kwa
ajili ya kuikabili Tanzania.
Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili Alhamisi ni walinda
mlango, Doukha Izeddine (JS Kabliye), M’bolhi Rais (Antalyaspor), Asselah Malik
(CR Belouizdad), walinzi Zeffane Mehdi (Rennes), Medjani Carl (Trabzonspor),
Ziti Mohamed (JS Kabliye), Mesbah Eddine (Sampordia), Bensebaini Ramy
(Montpeller), Belkarou Hichem (Club African), Ghoulam Faouzi (Namples), Mandi
Aissa (Reims).
Viungo ni Guedioura Adlane (Watford), Boudebouz Ryad
(Montpeller), Taider Saphir (Bologna), Abeid Mehdi (Panathinacos), Bentaleb
Nabil (Tottenham), Ghezzal Rachid (Lyon), Melsoub Walid (Lorient), Marhez Ryad
(Leicester).
Washambuliaji
Benrhama Said (Nice), Sliman Islam (Sporting Lisbon), Belfodil Ishak
(Beni Yas), Brahimi Yassine (FC Porto) na Bounedjah Baghdad (Etoile du Saleh)
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU NCHINI (TFF)


0 comments:
Post a Comment