![]() |
| Aaron Ramsey |
Klabu ya Arsenal sasa imepata habari njema za
kurejea dimbani kwa wachezaji wake watatu waliokuwa majeruhi.
Arsenal ilishindwa kupata matokeo mazuri katika
michezo miwili mfululizo dhidi ya Bayern Munich na Tottenham Hotspur.
Kuelekea michezo ya kimataifa ya kalenda ya FIFA,
Arsenal wamepata habari nzuri kutoka kwa wodi yao ya majeruhi baada ya taarifa
za kupona kwa winga Oxlade Chamberlain, Aaron Ramsey na mlinzi Hector Bellerin
ambao wanatarajiwa kurudi uwanjani baada ya wiki hiyo ya kimataifa.
Wachezaji hao mbali na Theo Walcott ambaye bado
hayuko sawa, wanatarajiwa kupangwa katika mchezo wa ligi kuu nchini humo dhidi
ya Westbromwich Albion wiki mbili zijazo.
Taarifa hizo ni nzuri kwa klabu ya Arsenal ambayo
wiki mbili zijazo itapigana kugombania nafasi ya kufuzu hatua ya 16 ya michuano
ya klabu bingwa barani Ulaya, mara baada ya kuwa imeshinda mchezo mmoja tu kati
ya minne iliyocheza.

0 comments:
Post a Comment