MALINZI ATOA 'BARAKA' KWA SAMATTA NA ULIMWENGU



Na Arone Mpanduka
Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Jamal Malinzi amewatakia kila lakheri wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Afrika itakayopigwa jioni ya leo kati ya TP Mazembe na USM Alger.

Mchezo huo utachezwa nchini Congo DR ambapo Mazembe itakuwa nyumbani kuialika Alger katika mchezo wa marudiano wa fainali.

Mechi ya kwanza iliyochezwa Algeria,TP Mazembe ilishinda 2-1 huku Mtanzania Mbwana Samatta akiifungia Mazembe bao la pili.

Samatta na Ulimwengu ambao ni wachezaji wa timu ya TP Mazembe, pia wanategemewa sana katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars.

Kufuatia hali hiyo Malinzi kupitia ukurasa wake wa twitter ameweka maneno ya kuwatakia mchezo mwema wachezaji hao katika mechi itakayoanza saa 10:30 jioni ya leo.

Maneno hayo yalisomeka: All the best @ulimwengu 11 and @Samatta 15 in todays CAFCL final.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment