SAMATTA AIPA UBINGWA TP MAZEMBE, ATWAA KIATU CHA DHAHABU














Mtanzania Mbwana Samatta leo ameweza kuipatia ubingwa wa Afrika klabu ya TP Mazembe baada ya kufunga bao kwenye mechi ya fainali dhidi ya USM Alger ya Algeria katika ushindi wa 2-0.

Mchezo huo ulichezwa nchini Congo DR ambapo Mazembe ilikuwa nyumbani kuialika Alger katika mchezo wa marudiano wa fainali.

Mechi ya kwanza iliyochezwa Algeria,TP Mazembe ilishinda 2-1 huku Mtanzania Mbwana Samatta akiifungia Mazembe bao la pili.

Samatta aliipatia Mazembe bao la kwanza katika dakika ya 74 kwa njia ya penati na kisha katika dakika ya 90 kutoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Assale.

Mazembe imetwaa ubingwa wa Afrika kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya ushindi wa awali wa 2-1 iliyoupata nchini Algeria.

Kufuatia bao moja alilofunga leo,Samatta amefikisha jumla ya mabao 8 katika mechi za Klabu Bingwa Afrika na kumfanya aongoze kwa ufungaji mabao.

Hiyo ina maana kwamba Samatta ameibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment