OLIMPIKI KUTUA MARACANA

Uwanja wa Maracana

















Shirikisho la soka duniani FIFA limeutangaza uwanja wa Maracana kuwa ndio utakaotumika katika fainali za michezo ijayo ya Olimpiki zitakazofanyika Brazil.

Mchezo wa ufunguzi wa makundi kwa wanawake utafanyika Agosti 3 mwakani katika Uwanja wa Olimpiki katika mji wa Rio de Janeiro.

Mchezo wa ufunguzi wa wanaume nao utafanyika Agosti 4 katika uwanja wa Brasilia, ambao ndio uwanja ghali zaidi kujengwa na ulitengenezwa kwa ajili ya Kombe la Dunia la lililofanyika nchi humo mwaka 2014.

Viwanja saba vitatumika katika michezo hiyo vikiwemo viwili katika mji wa Rio de Jeneiro, pamoja na Arenas ulioko Belo Horizonte, Brasilia, Manaus, Salvador na Sao Paulo.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment