Klabu ya soka ya Azam FC imekanusha taarifa ya
kupokea maombi kutoka katika klabu mbalimbali za ndani na nje ya nchi ya
kumuwania mchezaji wao Didier Kavumbagu katika dirisha dogo la usajili linalotarajiwa
kufunguliwa hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo Afisa
Habari wa Azam FC Jaffary Iddi amesema wao kama klabu bado hawajapata taarifa
yoyote kuhusu mchezaji huyo hivyo bado ni mali yao.
“Tumekuwa tukisikia taarifa za mchezaji huyo
zikizungumzwa sana, lakini sisi tunasema hazina ukweli wowote na Kavumbagu ni
mali yetu,” alisema Jaffary.
Kwa kipindi kirefu Kavumbagu amekuwa akikalia benchi
bila sababu ya msingi jambo ambalo hivi karibuni lilimfanya alalamike kwa
vyombo vyahabari akidai hatendewi haki na kocha Muingereza Stewart John Hall.

0 comments:
Post a Comment