TATU BORA BALLON D'OR YATAJWA

Hatimaye wachezaji Cristiano Ronaldo, Neymar na Lionel Messi wamefanikiwa kutinga kwenye orodha ya tatu bora ya wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia maarufu kama Ballon d'or.

Messi na Neymar wanakipiga katika klabu ya Barcelona wakati Ronaldo anakipiga Real Madrid.

Huo ni mchujo wa mwisho kutoka katika majina 23 ya awali.

Sherehe zenyewe za kusaka mwanandinga bora wa dunia zitafanyika mwakani Januari 11.

Kwa sasa tuzo hiyo inashikiliwa na Cristiano Ronaldo.

Hafla ya kutangaza majina hayo imefanyika hivi punde nchini Uswisi.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment