Arsenal usiku wa leo(Jumatatu Disemba 21) itashuka dimbani Emirates kuialika Manchester City katika mchezo mwingine wa Ligi kuu England.
Mchezo huo wa Jumatatu maarufu kama Monday Night Football utapigwa saa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Mechi hiyo ni kali na muhimu kwa sababu Arsenal anashuka dimbani akiwa anashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi akiwa na pointi 33 huku City ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 32.

0 comments:
Post a Comment