AUBAMEYANG AZIDI KUTISHA

Mshambuliaji raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang ameendelea kuibeba Borussia Dortmund.

Aubameyang amefunga moja ya mabao mawili wakati Dortmund ikiiangusha Augsburg kwa mabao 2-0 katika michuano ya Kombe la Ujerumani. Bao la pili lilifungwa na Henrikh Mkhitaryan.

Kwa ushindi huo timu yake imefuzu kucheza nusu fainali ya michuano hiyo huku yeye akiwa amefikisha mabao 18 katika mechi 16 na kuingia kwenye rekodi ya kuwa mmoja wa washambuliaji hatari kabisa.

Aubameyang ambaye ameingia tatu bora ya kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika akiwa na Yaya Toure na Andre Ayew sasa ni tegemeo la ufungaji mabao katika kikosi hicho maarufu 
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment