AZAM FC YAWAUA 'WANA LIZOMBE', MBEYA CITY YASHIKWA

Ligi Kuu soka Tanzania Bara imendelea leo nchini ambapo Azam FC imeshinda 2-1 dhidi ya wenyeji wao Majimaji FC ya Songea.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Majimaji,timu ya Azam FC ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli la kuongoza dakika ya 11 kupitia kwa mshambuliaji wao wa kimataifa wa Burundi anayekipiga katika klabu hiyo Didier Kavumbagu na Ame Ally 19, wakati Maji Maji FC walipata goli la kufutia machozi kupitia kwa Alex Kondo dakika ya 54.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Tanzania bara

JKT Ruvu 2 – 2 Coastal Union-Uwanja wa Karume Dar es salaam

Mbeya City 1-1 Mgambo JKT-Uwanja wa Sokoine Mbeya.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment