Kocha mkuu wa Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola amesema ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Guardiola ambaye Juni 2013 alisaini mkataba wa miaka mitatu katika klabu hiyo, ameamua kutangaza rasmi baada ya kuwepo kwa uvumi wa muda mrefu kuhusiana na hatma yake.
Kocha huyo amekuwa na mafanikio katika kila klabu aliyoifundisha ikiwemo Barcelona ambayo aliitumikia kwa kipindi cha miaka minne.
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti ndiye atakayechukua nafasi yake pindi atakapoipa kisogo Allianz Arena.
Guardiola anatajwa kutaka kwenda kuinoa klabu ya Manchester City ya Uingereza.

0 comments:
Post a Comment