AZAM YAPANIA USHINDI LEO

Wachezaji wa timu ya Azam FC wameifungia kazi Majimaji ya Songea kwa kuhakikisha wanashinda mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi yao kwenye Uwanja wa Majimaji, mjini Songea leo.

Kikosi cha timu ya Azam FC tayari kimeshatua mkoani Ruvuma tangu juzi saa 1 usiku na leo asubuhi walifanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Majimaji ili kuuzoea kabla ya kucheza na wenyeji wao hao leo saa 10 jioni.

Hata hivyo uwanja huo umeonekana kuwa kwenye hali mbaya sana katika sehemu ya kuchezea, jambo ambalo limelilazimu benchi la ufundi la Azam FC kubadilisha staili ya uchezaji kwa kutumia sana pasi chache na kupiga mipira mingi ya juu.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment