TANZANIA YAENDELEA KUSINDIKIZA MISS WORLD

Mrembo wa Hispania Mireia Lalaguna Royo ndiyo mshindi wa taji la urembo la dunia maarufu kama Miss World 2015.

Royo ametwaa taji hilo katika fainali zilizofanyika usiku wa Jumamosi(Dis 19) katika kisiwa cha Sanya nchini China.

Katika fainali hizo Tanzania iliwakilishwa na Lilian Kamazima ambaye hakuambulia chochote.

Mara zote Tanzania imekuwa ikijitokeza katika ushiriki wa fainali hizo bila mafanikio yoyote.

Kamazima aliwakilisha Tanzania katika mashindano hayo baada ya kukabidhiwa taji la urembo wa Tanzania na Sitti Mtemvu ambaye mwaka jana alikumbwa na sekeseke la kughushi umri.

Urussi imeshika nafasi ya pili kwenye fainali hizo kupitia kwa Sofia Nikitchuk huku nafasi ya tatu ikienda kwa nchi ya Indonesia kwa kutwaliwa na Maria Harfanti.

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment