BARCELONA BINGWA WA DUNIA

Barcelona wametwaa taji la tano katika michuano mbalimbali iliyoshiriki mwaka 2015 baada ya kuifunga River Plate ya Argentina mabao 3-0 na kunyakua taji la Dunia ngazi ya vilabu.

Mchezo huo wa fainali ulifanyika mchana wa leo huko nchini Japan.

Barcelona ameshiriki fainali hizo akiwa ni bingwa wa Ulaya ngazi ya vilabu.

Mabao matatu ya Barcelona yamefungwa na Messi (36'), Suárez (49', 68').

Katika mchezo huo, River Plate walionekana kushindwa kuimudu safu ya ushambuliaji ya Barca iliyoongozwa na Lionel Messi.

Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment