BENZEMA HATIHATI KUTOSWA TIMU YA TAIFA

Waziri mkuu wa Ufaransa Manuel Valls ametishia nafasi ya mshambuliaji Karim Benzema katika timu ya taifa ya Ufaransa kutokana na kushiriki tukio la video ya ngono alipoivujisha video hiyo inayomuonesha mshambuliaji mwenza Valbuena huku waziri huyo akisema wachezaji kama yeye lazima wawe ni kioo cha jamii.

Majuma kadhaa yaliyopita Benzema alikutwa na hatia ya kuvujisha video iliyomrekodi mchezaji mwenza Valbuena katika clip ya ngono ‘blackmail’ na sasa anaendelea kuchunguzwa na ingawa bado haijafahamika atapewa adhabu gani kutoka shirikisho la soka Ufaransa, tayari hofu ni kubwa huenda asiichezee tena timu ya taifa lake kutokana na utovu wa nidhamu.

Waziri mkuu huyo amesema Karim Benzema kama wachezaji wengine lazima wawe mfano wa kuigwa na kwamba mchezaji huyo hana nafasi tena katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.

Timu ya taifa ya Ufaransa inajiandaa na michuano ya mataifa ya Ulaya ‘EURO 2016′ huku wao wakiwa ndio waandaaji wa fainali hizo zitakazoshirikisha mataifa bingwa barani Ulaya.
Share on Google Plus

About MPANDUKA BLOG

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment