Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kupitia kipindi
chake maalumu cha uchunguzi, limeuona ushahidi kwamba rais wa FIFA Sepp Blatter
aliyesimamsishwa kwa muda anachunguzwa na shirika la ujajusi la Marekani FBI
kuhusiana na hongo ya dola milioni 100.
Kampuni ya masoko ya michezo inaaminika kulipa
mamilioni ya dola za Kimarekani kwa maafisa waandamizi wa FIFA katika miaka ya
mwishoni mwa 1990 ili kupewa haki ya kutangaza michuano ya kombe la dunia.
Aliyekuwa ameshika nafasi hiyo kabla ya Blatter,
Joao Havelange, alikuwa ni mmoja wa wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo.
Blatter, amekana kuwa na taarifa yoyote ya sakata
hilo, lakini kipindi cha Panorama kimeona barua iliyosainiwa na Joao Havelange
ikisema Blatter anazo taarifa kamili.

0 comments:
Post a Comment