Timu
ya Portland Timbers wametawadhwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya
Marekani-MLS kwa mara ya kwanza baada ya kuifunga Columbus Crew katika mchezo
wa fainali huku beki wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza Liam Ridgewell
akilibeba taji hilo.
Katika
mchezo huo Timbers walishinda kwa mabao 2-1 ambayo yalifungwa na Diego Valeri
pamoja na Rodney Wallace katika kipindi cha kwanza huku lile la kufutia mchozi
la Columbus likifungwa na Kei Kamara.
Nahodha
wa Timbers Ridgewell mwenye umri wa miaka 31, amewahi kucheza katika timu za
Ligi Kuu zikiwemo Aston Villa, Birmingham City na West Bromwich Albion.
Ushindi
huo unaifanya Timbers kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka alipojiunga na
MLS mwaka 2011.




0 comments:
Post a Comment